Baada ya TFF kuruhusu uwanja wa Azam Complex Kutumika katika mechi ambazo zitaihusisha Azam Fc dhidi ya Yanga na Simba yani Azam itakapokuwa Nyumbani basi msemaji wa Ruvu Shootoing Masau Bwire naye Aibuka na Kutaka Uwanja wao wa Ruvu Shooting (Uwanja wa Mabatini) kutumika dhidi ya Vigogo hao.
Masau Bwire amesema " Nina imani na TFF mpya kama wameanza na suala la Azam kuruhusiwa kutumia Chamazi basi hata Mabatini inabidi vigogo hawa Simba na Yanga waje wacheze, Maana sidhani kama suala la Usalama ni Kitu kinachoshindikana labda tu TFF waseme huwa wanahitaji mapato makubwa ila siyo usalama "
Na Kuhusu idadi ya Mashabiki Masau Bwire ndugu msomaji wa Kwataunit Blog amesema washabiki watakaowahi kukata tiketi ndiyo haohao wataingia kuangalia Mechi wala hilo siyo Tatizo.
Baadhi ya Vilabu Ruvu Shooting ikiwemo vimekuwa vikilalamika mara kadhaa kuhusiana na MICHEZO yao ya Nyumbani dhidi ya Vigogo wa soka Nchini Simba na Yanga Kupelekwa Uwanja wa Taifa licha ya kuwa na Viwanja vyao vya Nyumbani.
Ila Upande wa Mtibwa Sugar msomaji wa Kwataunit.com ambao wao hutumia uwanja wa Manungu Complex katika Mechi za Nyumbani lakini inapofika game za vigogo yani Simba na Yanga huamia Uwanja wa Jamhuri Morogoro wamesema Wao wataendelea na Utaratibu wao wa Awali wa Kucheza Manungu mechi nyingine lakini za Yanga na Simba watajisogeza Jamhuri.
No comments